Rais Dk. Mwinyi apokea pole kutoka kwa Shirika la Mzinga

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Mnazi Mmoja kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga kwa niaba ya uongozi wa shirika hilo,   kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

    Rais Dk. Mwinyi ameshukuru uongozi wa shirika hilo kwa kuja kumfariji.


Pia, Rais Dk. Mwinyi amepokea pole kutoka kwa Mh. Makamba 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Mnazi Mmoja kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Pia katika mazungumzo yao wamegusia shughuli za uendeshaji wa ofisi ya Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar.


Chapisha Maoni

0 Maoni