Rais apokea Ripoti ya CAG na Taarifa ya TAKUKURU

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/23 kutoka kwa Bw. Charles Kichere Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Machi, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2022/2023 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo CP. Salum Hamduni Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Machi, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kazi kubwa walioifanya kwa ufanisi mkubwa.

Dkt. Samia ametoa pongezi hizo leo Ikulu, baada ya kupokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/2023 pamoja na taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2022/2023.

Amesema kwamba ripoti hiyo ya CAG na taarifa ya TAKUKURU ni katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji ili yale yaliyotokea kwenye mchakato wa kuendesha Serikali, ambapo changamoto na mafanikio yanaainishwa vizuri, na huko ni kuimarisha uwajibikaji na uwazi.

“Uwekezaji tunaoufanya katika taasisi hizi pamoja na nyingine zilizokuwepo hapa zinafanya taasisi hizi kuaminiwa, kuaminiwa kwanza na wananchi kwa sababu leo wananchi wamesikia hali halisi ya uwendeshaji wetu wa kazi, ingawa ripoti hizi ni za awali, kunamajibu kutoka serikalini tutajibu mengine yaliyoonekana kuwa sio yatakuwa ndio,” amesema Dkt. Samia.

Katika Ripoti yake hiyo CAG, Charles Kichere amesema kumekuwa na mafanikio makubwa ambapo kwa mwaka 2022/2023 kuna asilimia 99 ya hati safi, hata hivyo ameeleza baadhi ya mashirika kuendelea kupata hasara, ukiukaji wa taratibu za manunuzi na malipo ya Serikali, pamoja na mambo mengine.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Hamduni amesema wamefuatulia miradi 12 ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji yenye thamani ya shilingi bilioni 107.4 katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, 

Chapisha Maoni

0 Maoni