Bochi kuanza kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF

 

Uongozi wa NHIF ukiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Dkt. David Mwenesano wametembelea na kukutana na uongozi wa Hospitali ya Bochi baada ya Hospitali hiyo kuandika barua ya utayari wa kuanza kuhudumia wanachama wa NHIF.

Hospitali iliyopo Jijini Dar es Salaam tayari imesaini mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa kitita kipya na huduma zimerejea kama kawaida kwa wanachama wa NHIF.

Hapo jana hospitali kadhaa za binafsi ziliandika notisi ya kusitisha kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF, wakisusia kitita kipya cha huduma za NHIF.

Chapisha Maoni

0 Maoni