Uzalishaji maji Ruvu Chini warejea katika hali ya kawaida leo

 

Kazi ya Marekebisho ya Pampu ya kusukuma maji katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini sasa imekamilika rasmi.

Marekebisho haya yaliyopelekea upungufu wa uzalishaji maji kutoka lita milioni 270 hadi lita milioni 220 kwa siku, na kusababisha uhaba wa maji katika maeneo mengi ya Dar es Salaam.

Matengenezo yamekamilika leo, Februari 26, 2024 na kurudisha hali ya uzalishaji katika kawaida yake ya ujazo wa lita milioni 270 kwa siku.

Taarifa iliyotolewa imesema kufuatia kazi hiyo kukamilika maeneo yafuatayo yataanza kupata huduma ya maji kwa msukumo mzuri. Maeneo hayo ni kama yafuatayo:-

Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba,  Mivumoni, Kawe,  Lugalo, Makongo,  Chuo,  Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay,  Masaaki,  Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe,  Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti,  Ilala na Katikati ya Jiji.






Chapisha Maoni

0 Maoni