Rais wa Poland Andrzej Duda awasili mchini kwa ziara ya siku mbili

 

Rais wa Poland Andrzej Duda na mkewe Agata Kornhauser-Duda amewasili nchini kwa ziara ya siku mbili na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrick Soraga na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Rais wa Poland Andrzej Duda na mkewe Agata Kornhauser-Duda wakipewa zawadi ya mashada ya maua na watoto baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, akimtambulisha Rais wa Poland Andrzej Duda viongozi mbalimbali waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, akizungumza na Rais wa Poland Andrzej Duda mra baada ya kumpokea katika uwanja uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba, Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrick Soraga wakiongea na Rais wa Poland Andrzej Duda.

Chapisha Maoni

0 Maoni