Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi ametoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye
bidhaa ya sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
kwa kutopanda bei ya bidhaa hiyo.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akizungumza na Wafanyabiashara
wa Soko kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi
tarehe:26 Februari 2024 katika ziara yake maalumu ya alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara
kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha
mara mbili ya bei ili kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan.
Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amewasisitiza Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.
0 Maoni