Rais Dk. Mwinyi ahimiza malezi bora katika jamii

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza malezi bora katika jamii ili kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya, wizi, ubadhirifu wa mali za umma, udhalilishaji na ulevi.

Rais Dk. Mwinyi amesema malezi bora yanaanzia ngazi ya familia, pia amewataka wazazi na walezi Kuwalea vijana katika malezi mema yenye maadili.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Makuti Kisiwandui Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 16 Februari 2024.

Rais Dk. Mwinyi ameshiriki katika ibada ya sala ya Ijumaa Misikiti mbalimbali Unguja na Pemba mpaka sasa idadi yake ni 133 pia amefungua Misikiti mipya 28 Unguja na Pemba.


Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi akisalimiana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu aliposhiriki katika ibada ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Makuti Kisiwandui Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 16 Februari 2024.


Chapisha Maoni

0 Maoni