Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha
tarehe 24 Februari, 2024, kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dodoma
imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mdogo wa Udiwani
katika kata 23 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 20 Machi, 2024 kwa asasi
za kiraia 11.
Kwa Mujibu wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyosainiwa na
Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima, R. K imeainisha Asasi za kiraia 11 ambazo
zimekidhi vigezo na kupewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura pamoja na kata
walizoomba kutoa elimu hiyo kuwa ni
Mbogwe Legal Aid Organization (MBOLAO) Isebya iliyopo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mbogwe, Sustainable Hub for Policy Initiatives (SHPI) Mshikamano
iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.
Asasi zingine ni Promotion and Women Development Association
(PWDA) Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji,
Bagamoyo Community Capacity Empowerment and Education (BCCEE) Fukayosi iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Action for Democratic Governance
(A4DG) Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Asasi zingine ni Vanessa Foundation ambayo itatoa elimu
katika kata ya Nkokwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Tanzania
Centre for Disability Development Initiatives (TCDDI) Nkokwa iliyopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Safe Society Platform Tanzania (SSPT) Busegwe
iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama na Isebya iliyopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
Asasi zingine za kiraia zilizopata kibali ni Youth Against
Aids and Poverty Association (YAAPA) ambayo itatoa elmu katika kata ya
Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Musoma
Municipal Paralegal Organisation (MMPO) Mshikamano iliyopo katika Halmashauri ya
Manispaa ya Musoma.
Asasi nyingine iliyopata kibali ni Shirika la Elimu ya Uraia
na Uzalendo “Civic Education and Patriotism Association” iliyoomba kutoa Elimu
katika kata za Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni,
Msangani iliyopo katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Fukayosi iliyopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlanzi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Kibiti na Kibata iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Wakati huo huo, Tume pia imetoa kibali kwa asasi za kiraia
tatu ambazo zimekidhi vigezo ili ziweze kutazama uchaguzi mdogo wa Udiwani
katika Kata 23 za Tanzania Bara.
Asasi hizo tatu zitakazoenda kutazama uchaguzi Mdogo wa
udiwani siku ya Jumatano tarehe 20 Machi, 2024 ni Tanzania Alliance for
Disability Development Initiatives itakayokuwa katika kata ya Mhande iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Bridge Development Trust Organisation
itakuwa katika kata ya Buzilasoga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Sengerema na Promotion and Women Development Association itayokuwa katika Kata
ya Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Aidha, katika kikao hicho, Tume imezitaka asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura, kuzingatia Mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura wa Mwaka 2020 katika kipindi chote cha kutoa elimu hiyo katika uchaguzi mdogo.
0 Maoni