Mjane aliyehukumiwa miaka 22 jela kwa nyama ya swala aachia huru

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Irvin Mgeta, amemuachia huru Mjane Maria Ngoda aliyehukumiwa kifungo cha miaka 22 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na vipande 22 vya nyama ya swala.

Jaji Mgeta ametoa uamuzi huo leo, na kueleza kuwa rufaa ya mjane huyo ilikuwa na hoja 13 zilizotolewa na upande wa mawakili wa rufaa, hoja ambazo zilionyesha mashtaka yaliyotolewa dhidi ya Maria hayakuthibitishwa na Mahakama iliyotoa hukumu yake.

Rufaa ya Mjane Maria Ngoda, iliyomnusuru na kifungo cha miaka 22 jela, ilisimamiwa na Mawakili wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa.

Chapisha Maoni

0 Maoni