Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PIC yaipongeza STAMICO

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imetembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichopo jijini Mwanza na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi.

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deus Clement Sangu imeona maendeleo mazuri ya usafishaji wa dhahabu kiwandani hapo ikilinganishwa na kipindi  cha nyuma walipotembelea kiwandani hapo.

Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ameipongeza Serikali  kupitia STAMICO  kwa  kuongeza mapato yake pamoja na kuanzisha kiwanda hicho ambacho kitapelekea  STAMICO kupata mapato na nchi kupata  faida mbalimbali kutokana  na usafishaji wa  dhahabu nchini.

Katika wasilisho lake la kamati Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO   Dkt Venance Mwasse alielezea utekelezaji  wa shughuli za kiwanda pamoja na changamoto  ya kiwanda  ya  kutokupata dhahabu ghafi   kwa wingi kutokana  na maswala mbalimbali ikiwemo changamoto ya kikodi.

Kamati iliahidib kuifanyia kazi changamoto hii ya kikodi kwa kushirikiana na Serikali ili kiwanda kiweze kupata malighafi ya kutosha na kufanya kazi vizuri.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO  Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo aliishukuru kamati ya PIC kwa ushauri wao wanaoutoa mara kwa mara kwa  Shirika kuhusu maswala ya uwekezaji  nakupelekea  Shirika kuendelea kufanya  vizuri.

Ziara   hii ya Kamati itahusisha kutembelea miradi mingine ya Shirika ya STAMIGOLD na Makaa ya mawe Kiwira ili  wajumbe wajionee uwekezaji wa STAMICO  katika miradi mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni