Wenyeji Ivory Coast waanza kwa ushindi AFCON

 

Wenyeji Ivory Coast wameanza kwa ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya AFCON 2023 kwa kuichapa Guinea-Bissau magoli 2-0.

Seko Fofana aliwafungia tembo hao goli la kwanza katika mchezo huo wa kundi A huko Abidjan kwa kutikisa nyavu katika dakika ya nne tu ya mchezo.

Fofana karibu afunge bao la pili kabla ya mapuziko hata hivyo shuti lake kali lilipanguliwa na kutolewa nje na Ouparine Djoco.

Alikuwa Jean-Philippe Krasso aliyepachika goli la pili la Ivory Coast baada ya mapumziko kwa kumiliki mpira vyema akiwa kwenye presha katika sanduku na kufunga.






Chapisha Maoni

0 Maoni