Timu ya Simba yateuliwa kuwa Balozi wa Utalii Zanzibar

 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Mohammed Said ameiteua timu ya Simba Sports Club kuwa Balozi wa Utalii visiwani humo.

Hatua hii inafuatia klabu ya Simba kuonyesha dhamira ya kutangaza utalii wa Zanzibar kupitia kauli mbiu ya Visit Zanzibar katika jezi zao pamoja na mitandao ya kijamii wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mtendaji Mkuu wa Simba Iman Kajula imeishukuru Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar kwa kutambua mchango wa Klabu ya Simba kwa kutangaza utalii Zanzibar pamoja na kusaidia kuipa hadhi ya Kimataifa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Chapisha Maoni

0 Maoni