Simba kuyapa hadhi ya kimataifa Mapinduzi CUP

 

Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally amesema klabu hiyo imeamua kuyabeba mashindano ya Mapinduzi Cup ili kuyapa thamani ambayo itaifanya kila timu Afrika itamani kushiriki, ione raha kuja Zanzibar.

“Kuanzia mechi ya kesho dhidi ya Singida Fountain Gate tutavaa jezi zenye nembo ya Zanzibar. Ndani ya siku hizi 14 za kuchukua ubingwa wa Mapinduzi tutatembelea maeneo ambayo yana vivutio vizuri lakini havionekani sana, sisi tutaitangaza kupitia kwenye kurasa zetu,” amesema Ally.

Lengo letu ni moja tu kuongeza namba ya watalii hapa visiwani Zanzibar. Nawaomba Wanasimba tukitangaza sehemu ambayo tunatembelea mjitokeze kwa wingi, amesema Ally. #UchumiWaBuluu #VisitZanzibar #WenyeNchi #NguvuMoja

Chapisha Maoni

0 Maoni