Anayedaiwa kumuua kwa kumchoma visu mpenzi wake afariki dunia

 

Lucas Tarimo, mtuhumiwa anayedaiwa kumchoma kisu mara 25, Beatrice Minja na kumsababishia kifo, amefariki dunia akiwa chini ulinzi wa Jeshi la Polisi akipatiwa matibabu hospitalini Wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Taarifa za kifo cha Lucas, zimethibitishwa na Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Huruma wilayani Rombo Daria Mushi, ambaye amesema mthuhumiwa huyo amefariki dunia jana majira ya saa 4:30 usiku.

Marehemu Lucas alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa amejificha katika Kijiji cha Jema Kata ya Oldonyo Sambu Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha akijiandaa kukimbilia nchi jirani, baada ya kufanya tukio hilo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, alisema kuwa marehemu baada ya kuona mkono wa Serikali unamfikia alikunywa sumu inayotumika kuua wadudu ambapo baada ya kukamatwa alikimbizwa hospitali.

Novemba 12, 2023 marehemu Lucas alidaiwa kumchoma kisu mara 25 marehemu mkewe Beatrice Minja, ambaye alikimbizwa hospitali na kukaa ICU siku 46 katika Hospitali ya KCMC na baadae akafariki dunia.

Chapisha Maoni

0 Maoni