Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa China Mhe. Zhang
Zhisheng anayefanyia kazi zake Zanzibar, kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa
utumishi nchini tarehe 29 Januari 2024, Ikulu Zanzibar.
Aidha Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Balozi Mhe. Zhang Zhisheng
kwa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zanzibar na China
katika miaka mitatu ya utumishi wake nchini, pia kwa kuratibu vema ziara yake
mwaka jana China.
Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa China imeendelea
kusaidia Zanzibar na kushirikiana katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo
sekta ya afya kwa kuleta madaktari
kutoka China, ufadhili wa masomo, kujengea uwezo, biashara, utalii,
pamoja na kuwepo kwa kampuni za kichina
katika kazi za miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara, bandari, na uwanja
wa ndege.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amewakaribisha wawekezaji
kutoka China kwenye sekta ya utalii kujenga hoteli kwa kuongeza watalii zaidi
wa Kichina kuitembelea Zanzibar.
Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na
kudumisha uhusiano na China ambayo yametimiza miaka 60.
Naye Balozi Mhe. Zhang Zhisheng amesema China itaendelea kushirikiana na Zanzibar kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.
0 Maoni