Mapokezi ya Rais Samia Ikulu ya Indonesia

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la heshima wakati wa mapokezi yake Rasmi katika viwanja vya Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Waandishi wa Habari pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace nchini humo tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinawishwa mikono na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo mara baada ya kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea masuala mbalimbali ya ziara yake nchini Indonesia tarehe 25 Januari, 2024. Pembeni ni mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo.

Chapisha Maoni

0 Maoni