Kenya Airways yazuiliwa safari za Tanzania

 

Mamlaka ya Usimamizi wa Anga Tanzania (TCAA) imelifutia Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kibali cha kufanya safari zake za ndege nchini Tanzania kuanzia Januari 22, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Mkurungezi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari inasema kuwa mamlaka hiyo imefikia uamuzi huo kujibu hatua ya nchi ya Kenya kuinyima kibali Tanzania kusafirisha mizigo kwa njia ya anga kutokea nchini humo kwenda maeneo mbalimbali duniani.

Hivyo basi, kuanzia Januari 22, 2024 hakutakuwa na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya itakayofanya safari zake kati ya Nairobi na Dar es Salaam, imesema taarifa hiyo.

Shirika la Ndege la Kenya KQ hufanya safari za ndege 33 kati ya Nairobi na Dar es Salaam kwa wiki.



Chapisha Maoni

0 Maoni