Dkt. Mpango apokea taarifa ya uandishi wa kitabu cha miaka 60 ya ofisi yake

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na kuwasilisha taarifa ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘, Januari 05, 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Dkt. Harrison Mwakyembe - Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘ mara baada ya kupokea taarifa ya uandishi wa kitabu hicho ofisini kwake Ikulu mkoani Dodoma Januari 05, 2024. Wengine wa pili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga, Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa Kitabu Bw. Rawson Yonazi na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano – Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘ Bw. Rawson Yonazi (wa kwanza kulia) baada ya kupokea taarifa ya uandishi wa kitabu hicho ofisini kwake Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Januari 05, 2024. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi wa kitabu cha ‘Miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais‘ Bw. Rawson Yonazi, (kulia) Makamu Mwenyekiti Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu baada ya kamati hiyo kuwasilisha taarifa ya uandishi wa kitabu hicho ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Januari 05, 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni