Viongozi wa Sekta ya Utalii Zanzibar wapatiwa uzoefu wa kiutendaji TANAPA

 

Viongozi wa Sekta ya Utalii Zanzibar wakiongozwa na Dkt. Abdulla Mohamed Juma, Mkurugenzi wa Utalii Zanzibar wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Viongozi hao wamefanya ziara hiyo Jijini Arusha leo tarehe 28.12.2023 kwa lengo la kujifunza mbinu na mikakati ya kuboresha sekta ya Utalii na kupata uzoefu wa kuimarisha ulinzi na usalama wa watalii wanaotembelea vivutio vya Utalii.

TANAPA imeendelea kuwa na ulinzi imara wa wageni na mali zao kwa watalii wanaotembelea Hifadhi za Taifa na kupelekea kuwa sehemu muhimu kwa taasisi nyingi kwenda kujifunza ili kupata uzoefu.



Chapisha Maoni

0 Maoni