Mwanamuziki wa Afrika Kusini Zahara Afariki Dunia

Mwanamuziki nyota wa muziki wa Afro-pop Bulelwa Mkutukana, maarufa kama Zahara, amefariki dunia, Waziri wa Utamaduni wa Afrika Kusini ametangaza.

Nyota huyo mshindi wa tuzo kadhaa, alikuwa amelazwa hospitali akisumbuliwa na tatizo la ini, na Serikali ilikuwa ikiisaidia familia yake, Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Zizi Kodwa amesema.

Zahara alipata umaarufu mnamo mwaka 2011 kupitia album yake ya Loliwe, iliyopendwa sana katika mataifa mbalimbali ya Afrika.

Mnamo mwaka 2019, Zahara alivunja ukimya na kuongelea tatizo la uraibu wa pombe lililokuwa likimsumbua. 

Mwezi uliopita, familia yake ilithibitisha Zahara kulazwa hospitali na kuwaomba wananchi wa Afrika Kusini kumuweka mwanamuziki huyo kwenye maombi.

Zahara amefariki dunia usiku wa Jumatatu kwenye hospitali moja Jijini Johannesburg akiwa na umri wa miaka 36, tovuti ya habari ya SABC imeandika.

Chapisha Maoni

0 Maoni