Mama na watoto wake wanne wauawa Paris

 

Polisi nchini Ufaransa wameanza kuchunguza tukio la mauaji baada ya miili ya watu watano kukutwa kwenye jengo la ghorofa mashariki mwa Jiji la Paris.

Miili iliyobainika ni ya mwanamke mmoja pamoja na watoto wake wanne wenye umri wa kati ya miezi tisa na 10, waendesha mashtaka wamesema.

Miili hiyo imebainika jana majira ya jioni kwenye mji wa Meaux, kilomita 40km kutoka kwenye Jiji la Paris.

Polisi walikuwa wanamtafuta baba mwenye umri wa miaka 33 na hii leo wamemkamata mwanaume mmoja.

Chapisha Maoni

0 Maoni