Matukio mbalimbali Ikulu ya Dar es Salaam leo

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Maryam Ahmed Muhaji kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana,  Kamishna wa Maadili Jaji Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Ndugu Majula Mahendeka, Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Sendega na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Tanzania Startup Association (TSA) ikiongozwa na Mwenyekiti wao Ndugu Paul Makanza pamoja na Wajumbe aliofuatana nao walipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tanzania Startup Association (TSA) Ndugu Paul Makanza, Mtendaji Mkuu Ndugu Zahoro Muhaji na Makamu Mwenyekiti, Ndugu Lulu Ng’wanakilala pamoja na Wajumbe waliofuatana nao mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Desemba, 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni