Kamati ya HMTH yajitambulisha kwa Katibu Mkuu Abdulla

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amekutana na Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo leo ofisini kwake jijini Dodoma.

Lengo la kikao hicho ni kuitambulisha kamati hiyo kwa Katibu Mkuu Abdulla ambapo miongoni mwa majukumu ya Kamati hiyo ni pamoja na kumshauri Afisa Masuuli katika masuala ya Udhibiti wa ndani, Usimamizi wa vihatarishi, Mfumo wa kiutawala na kupitia na kushauri kuhusu hoja na mapendekezo yanayotolewa na Mkaguzi wa Ndani, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seikali (CAG) na Mamlaka nyingine kama vile PPRA.

Pia kamati imeainisha baadhi ya majukumu yake ikiwemo kupitisha mpango wa ukaguzi wa ndani, kutoa ushauri kuhusu uandaaji wa hesabu za Wizara na kupitia na kushauri hatua za utekelezaji wa mapendekezo yanayotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Kamati hiyo ina wajumbe watano, Katibu wa kamati pamoja na sekretarieti ya Kamati yenye idadi ya watu wanne.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Bwana Christopher Nkupama  ambae ni Mwenyekiti, Bwana Erick Kitali, Bwana Priscus Kiwango, Bwana Mulembwa Munaku na Bwana Elisa Mbise.

Pia kamati hiyo imeainisha baadhi ya majukumu yake ikiwemo kupitisha mpango wa ukaguzi wa ndani, kutoa ushauri kuhusu uandaaji wa hesabu za Wizara na kupitia na kushauri hatua za utekelezaji wa mapendekezo yanayotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Kamati hiyo ina wajumbe watano, Katibu wa kamati pamoja na sekretarieti ya Kamati yenye idadi ya watu wanne.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Bwana Christopher Nkupama  ambae ni Mwenyekiti, Bwana Erick Kitali, Bwana Priscus Kiwango, Bwana Mulembwa Munaku na Bwana Elisa Mbise.

Chapisha Maoni

0 Maoni