Jela miezi sita kwa kuangusha ndege ili kupata views nyingi

 

Mtumiaji youtube amehukumiwa miezi sita jela kwa kuangusha ndege kwa makusudi ili kupata watazamaji wengi (views), na kuwadanganya wachunguzi wa ajali wa Marekani.

Trevor Jacob, 30, aliiposti video ya ndege ikianguka Desemba 2021, akidai kuwa ni ajali, na kuruka kutoka kwenye ndege akijichukua picha za selfie huku akishuka chini kwa parachuti

Video hiyo ya ajali ya kupangwa ilitazamwa mara nyingi na mamilioni ya watu kwenye youtube channel yake.

Katika makubaliano ya kukiri kosa hilo, Jacob alisema kuwa alipiga picha ya ajali hiyo ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya udhamini wa bidhaa.



Chapisha Maoni

0 Maoni