Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe.
Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli Ikulu
Zanzibar aliyefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Disemba
2023.
Rais Dkt. Mwinyi amesema
Zanzibar sekta kuu ya uchumi ni utalii ni fursa kwa Uganda kufanya
biashara na uwekezaji pamoja na fursa
nyingine zilizomo katika uchumi wa buluu .
Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amemtaka Balozi Simuli
kudumisha ushirikiano na kubadilishana taarifa za ulinzi na usalama eneo la
mpakani kati ya Tanzania na Uganda.
Naye Balozi Simuli amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kazi
nzuri anayoifanya kuibadilisha Zanzibar kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.
🗓️28 Disemba 2023
📍Ikulu, Zanzibar.

0 Maoni