Cristiano Ronaldo afikisha magoli 1,200 katika soka

 

Cristiano Ronaldo amefikisha magoli 1,200 katika mechi zinazotambulika rasmi kimataifa kwenye mchezo wa soka baada ya kufunga goli moja na kusaidia jingine moja kwa timu yake ya Al-Nassr.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38, aliunganisha ndani ya nyavu mpira wa krosi uliopigwa na Sadio Mane, na baadae akamtengenezea goli Otavio katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al-Riyadh.

Ronaldo alitumia ushindi huo kuwashukuru wale wote waliomsaidia katika kufikisha rekodi hiyo, na kuongeza kwa kusema kuwa bado hajamaliza.

Mshambuliaji huyo raia wa Ureno anaongoza kwa ufungaji katika Ligi ya Saudi, akiwa ametikisa nyavu mara 16 katika mechi 15 kwenye msimu huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni