Mtanzania aliyefia Israel kuzikwa leo Rombo

 

Mwili wa Mtanzania Clemence Mtenga mwenye umri wa miaka 22, aliyeuawa vitani nchini Israel unazikwa leo nyumbani kwao katika Kijiji cha Kirwa, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Novemba 17, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilithibitisha kupokea taarifa za kifo cha Mtenga, ambaye alikuwa miongoni mwa Watanzania wawili waliokuwa hawajulikani walipo baada ya kuanza kwa vita kati ya Hamas na Israel.

Marehemu Clemence alikuwa miongoni mwa vijana 260 raia wa Tanzania waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo, chini ya mpango wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.

Chapisha Maoni

0 Maoni