Washiriki wa Tamasha la Ulimbwende la Viziwi watembelea Mikumi

 

Bodi ya Utalii Tanzania kupitia Mradi wa REGROW imeongoza watalii 165 wa umoja wa watu wenye usikuvu hafifu kutoka nchi 40 ambapo wamepata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Vivutio vya Utalii vya Tanzania vina miundombinu rafiki inayowawezesha watu wenye mahitaji maalum kuvimbelea na kufurahia uzuri wa vivutio vya Utalii vya asili vya Tanzania.


Wakiwa hapa nchini wameweza kufanya kongamano pamoja na kuendesha Mashindano ya Ulimbwende na Utanashati Miss & Mister Deaf International 2023 ambayo yamefanyika tarehe 25/11/2023 jijini Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

0 Maoni