Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema wakati wa kuadhimisha miaka 3 ya uongozi wake azma yake ya kuifungua Pemba kiuchumi inakwenda vizuri.
Dk. Mwinyi aliahidi
kuifungua Pemba kibiashara na uwekezaji kupitia maeneo makuu manne ikiwemo
mkakati wa kuboresha bandari za Pemba ambao unaendelea, ujenzi wa barabara,
kuvutia uwekezaji wa viwanda eneo la Chamanangwe yote yatatimia kabla ya
uchaguzi mkuu 2025.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo
akindua boti mpya ya Zanzibar 3 ya Kampuni ya Zan Fast Ferries itakayofanya
safari zake Pemba hadi Unguja kwa muda wa saa mbili, Tanga na Dar es Salaam bandari
ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 01 Novemba, 2023.
Rais Dk. Mwinyi amesema
alizungumza na wawekezaji mbalimbali kuhusu changamoto ya usafiri Pemba wa anga
na bahari hatimaye wawekezaji hao wameitikia wito ikiwemo Kampuni ya Azam
Marine, na leo Zan Fast Ferries kuileta boti mpya ya Zanzibar 3 kwa safari za
Pemba. Pia kampuni za Flight link na Assalam Air kuongeza ndege kwa safari za
Pemba.
0 Maoni