Baba jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wake wa kumlea

 

Mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Samson Mibulo (35), Mkazi wa kijiji cha Nyamizeze wilayani Sengerema baada kukiri kosa la kubaka.

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 122/2023, imetolewa leo tarehe 02 Novemba 2023 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Evod Kisoka.

Awali, akisoma maelezo ya kosa hilo mbele ya Hakimu, Wakili wa Serikali, Morice Mtoi amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo kwa mhanga kwa nyakati tofauti Okktoba 23 mwaka huu huku wakati akitambua kuwa nyeye ni baba mlezi wa mtoto huyo.

Mshtakiwa alikamatwa tarehe 23/10/2023 na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya ya Sengerema, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Tito Mohe baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Wakili wa Serikali, Morice Mtoi amesema mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na Kifungu namba130(1) (2)(e) na 131(1) cha Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 Toleo la mwaka 2022

Pamoja na maombi ya mshtakiwa (Mibulo) kuomba kupunguziwa adhabu, Mahakama imemhukumu kifungo hicho cha miaka 30 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni