Gharama ya cheti cha kumiliki gari la familia nchini
Singapore imeongezeka na kufikia rekodi ya juu ya dola 106,619, sawa na
shilingi 266,929,622 za Tanzania.
Serikali ya nchi hiyo ilianzisha mfumo wa malipo ya cheti
cha umiliki gari kwa muda wa miaka 10 (COE) mnamo mwaka 1990 ikiwa ni sheria ya
kukabiliana na msongamano wa magari.
Mtu anayetaka kumiliki gari nchini Singapore anapaswa kuwa
na cheti hicho cha COE, ili apatiwe ridhaa ya kununua gari.
Vyeti hivyo huuzwa kwa mnada kila baada ya wiki mbili, huku Serikali
ya Singapore ikidhibiti idadi ya vyeti vinavyouzwa.
Kwa kodi na ushuru wa forodha, mfumo huo umeifanya nchi ya
Singapore kuwa nchi ghali mno duniani kwa mtu kununua gari.
CHANZO: BBC
0 Maoni