Ronaldo aiongoza Ureno kuichakaza Bosnia

 

Cristiano Ronaldo amefunga magoli mawili wakati Ureno ikiichakaza Bosnia-Herzegovina magoli 5-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2024.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, aliifanya Ureno kuongoza kwa mkwaju wa penati kabla ya baadae kufunga goli lake la kimataifa la 127, na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Katika mchezo huo Ureno ambao walikuwa ugenini walifunga magoli hayo matano kabla ya mapumziko kupitia kwa Bruno Fernandes, Joao Cancelo na Joao Felix.

Kwa matokeo hayo Ureno ambayo ilishafuzu Euro 2024 tangu siku ya Ijumaa, inabakia kileleni mwa kundi J ikiwa na ushindi wa asilimia 100.

Chapisha Maoni

0 Maoni