Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujeruman Mhe. Dkt Frank Walter Steinmeier anatarajiwa kutembelea Makumbusho ya Kumbukumbu ya Vita vya MajiMaji Songea kesho tarehe 1 Novemba 2023 kwa lengo la kutoa heshima kwa mashujaa wa vita hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas amesema
maandalizi ya kuupokea ugeni huo yamekamilika ambapo baada ya kufika uwanja wa
ndege wa Songea ataenda moja kwa moja katika Makumbusho ya Vita vya MajiMaji.
Amesema akiwa katika Makumbusho hiyo atapata historia ya
makumbusho hiyo na kutoa heshima kwa mashujaa waliokufa katika vita hivyo
vilivypiganwa mwaka 1905 mpaka 1907.
Kanali Thomas ameongeza kuwa pamoja na kutoa heshima kwa
mashujaa wa Vita vya Majimaji Rais huyo wa Ujerumani atakutana na baadhi ya
wahanga wa vita hivyo na kisha kuelekea Shule ya Msingi MajiMaji.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Kamshna Benard Wakulyamba amesema kuwa kwa upande wa Wizara ya Maliasili ikiwa
ni pamoja na Makumbusho ya Taifa la Tanzania ambao ndio wasimamizi wa
Makumbusho ya Vita vya MajiMaji maandalizi yamekamilika kwa ajili ya kumpokea
Rais huyo wa Ujerumani.
Kamishna Benedict Wakulyamba, ameongeza kuwa ziara hiyo ya
Rais wa Ujerumani katika Makumbusho ya Majimaji licha ya kuimarisha mahusiano
ya kimataifa pia itakuwa chachu ya kuongeza utalii nchini.
0 Maoni