Rais Samia aanza ziara ya Singida; azindua shule ya Imbele

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Sagara mara baada ya kuwasili Mkoani Singida kwa ajili ya ziara ya kikazi tarehe 15 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa kuashiria ufunguzi wa Shule ya Msingi Imbele, mabweni ya madarasa ya Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Manispaa ya Singida Mjini tarehe 15 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Shule ya Msingi Imbele mara baada ya hafla ya ufunguzi Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mara baada ya kukagua moja ya Darasa la Shule ya Msingi Imbele wakati wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiimba pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Imbele mara baada ya kuwasili Shuleni hapo kwa ajili ya ufunguzi wakati wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni