Israel kufanya mashambulizi ya aridhini, anga na majini Gaza

 

Jeshi la Israel linapanga kuanza kufanya mashambulizi ya aridhini, angani na baharini katika eneo la ukanda wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewaambia wanajeshi kuwa mashambulizi ya aridhini yanatarajiwa kuanza, na kuongeza kuwa “hatua inayofuata inakuja”.

Israel imewaonya Wapalestina milioni 1.1 wanaoishi kaskazini mwa Gaza kuondoka kupitia kusini na maelfu wamekuwa wakikimbia vita kwa kutumia magari.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limelaani amri ya watu kuondoka Gaza na kusema hali ya kulazimisha wagonjwa waliopo hospitalini kuondoka ni sawa na hukumu ya kifo.

Chapisha Maoni

0 Maoni