Rais Joe Biden kutembelea Israel Jumatano

 

Rais wa Marekani Joe Biden atatembelea Israel Jumatano kupatiwa taarifa ya mipango ya vita dhidi ya wapiganaji wa kundi la Hamas.

Marekani imesema Rais Biden ataelezwa namana Israel itakavyofanya oparesheni katika namna ambayo itapunguza madhara kwa raia.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, amesema Washington imefanikisha kuhakikishiwa na Israel kuruhusu kuingizwa misaada ya kibinadamu Gaza.

Taarifa zaidi zinasema maelfu ya watu wa Gaza wamekusanyika kwenye mpaka wa Rafah ili kuingia Misri wakati jitihada za Kidiplomasia zikiendelea kufungua mpaka huo, kabla ya kuanza vita ya aridhini.

Chapisha Maoni

0 Maoni