Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi amesema mbio za Marathon zina faida ya kiafya, ajira na
uchumi.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika msimu wa tatu wa
mbio za Zanzibar International Marathon kuanzia kilometa 5, 10 na 21 zilizoshirikisha
wakimbiaji wa nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, Ulaya na Amerika leo tarehe
29 Oktoba 2023 eneo la Forodhani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha Rais Dk. Mwinyi ameeleza katika kuvutia wageni kipindi
chote cha msimu mdogo wa watalii tuwe tuna utalii wa matukio ikiwemo Tamasha la
ZIFF, Sauti za Busara, pamoja na matukio ya kimichezo ikiwemo mbio za Zanzibar
International Marathon kwa kuhamasisha kufurika wageni vipindi vyote msimu
mkubwa na mdogo wa utalii.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi ametoa wito kwa wananchi kufanya
mazoezi kila wakati kwa kujiunga na vikundi vya mazoezi kukabiliana na magonjwa
yasiyoambukiiza yakiwemo shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo,
saratani, kiharusi na mengineyo.
Pia viongozi mbalimbali wa Serikali wa SMT na SMZ pamoja na
wadau wa taasisi binafsi na michezo wameshiriki mbio hizo.
0 Maoni