Netanyahu aahidi kuua kila mwanachama wa Hamas

 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa kila mwanachama wa Hamas atauawa, kauli ambayo ameitoa baada ya mkutano wa kwanza wa dharura wa serikali.

Akiwa pamoja na kiongozi wa kambi ya upinzani Benny Gantz, Netanyahu amesema kuwa ni muda wa vita sasa.

Hata hivyo, Rais Joe Biden wa Marekani ameongea na Netanyahu na kumueleza wazi Israel inapaswa kuzingatia sheria za vita.

Vifo vilivyotokea Israel vimefikia watu 1,200, huku nako watu zaidi ya 1,100 wameuawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Chapisha Maoni

0 Maoni