Mike Pence achemsha katika mbio za urais Marekani

 

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, amejitoa kwenye mbio za kinyang’anyiro cha urais wa Marekani 2024, akisema kwamba huu si wakati wake.

Pence aliyekuwa Makamu wa Rais wakati wa utawala wa Rais Donald Trump, ametangaza kujitoa kwenye kongamano la wanachama wa Republican Wayahudi huko Las Vegas, Jumamosi mchana.

Pence anakuwa mgombea wa kwanza mwenye jina kubwa wa chama cha Republican kusitisha kampeni zake katika mbio za urais ambazo kwa chama hicho Donald Trump bado anaongoza.

Makamu huyo wa rais wa zamani wa Marekani, amekuwa hafanyi vyema kwenye kura za maoni na pia amekuwa akishindwa kupata kura za wanachama wa Republican.

Chapisha Maoni

0 Maoni