Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt.
Philip Isdori Mpango amekabithi Hati ya Hakimiliki za Kimila kwa wananchi wa
Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe.
Dkt. Mpango amekabidthi hati saba za mfano kati ya
Hatimiliki za Kimila 6,883 zilizoandaliwa tarehe 27 Oktoba 2023 katika halfa
iliyofanyika Kijiji cha Tandala Wilayani humo akiwa katika ziara yake ya kikazi
ya siku tatu mkoa wa Njombe.
Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amesema, utolewaji Hati za Kimila
wilayani Makete unafuatia uwezeshwaji uandaaji mipango ya matumizi bora ya
ardhi uliofanywa na wizara yake kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi
Bora ya Ardhi katika vijiji.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda mkoa wa Njombe una jumla ya vijiji
323 ambapo vijiji 264 kati ya hivyo tayari vimewezeshwa kuandaliwa mpango wa
matumizi bora ya ardhi.
"Mhe Makamu wa Rais mkoa wa Njombe tunavyo vijiji 323
na kati ya hivyo vijiji 295 tayari vimewezeshwa na sasa tuko katika wilaya ya
Makete kama taarifa ilivyoeleza" alisema Mhe. Pinda.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete
Bw. William Makufwe amesema kuwa, upatikanaji wa Hatimiliki hizo ni jitihada za
Wilaya kukuza zao la ngano à lilolieleza kuwa linazalishwa kwa wingi katika
Wilaya hiyo.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa, Wilaya yake imeamua
kuendesha kilimo cha zao hilo Kimkakati kwa kupima na kumilisha mashamba
kupitia Hatimiliki za Kimila ili ziwape fursa wakulima ya kuongeza mitaji
itakayoinua wigo wa uzalishaji zao
hilo.
Ugawaji wa Hatimiliki hizo unafuatia kazi iliyofanywa na
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Tume ya Taifa ya Mipango
ya Matumizi ya Ardhi iliyowezesha uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya
Vijiji 64 katika wilaya ya Makete na kutoa jumla ya Hatimiliki za Kimila 6,889.
Kazi hiyo imetekelezwa katika awamu mbili ambapo, wamu ya
kwanza, ilihusisha uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji 44 na
upimaji wa vipande vya ardhi katika vijiji 17 ambapo jumla ya hati 6,594
ziliandaliwa.
Aidha, katika awamu ya pili uandaaji wa mipango ya matumizi
ya ardhi ya vijiji 20 kwenye Tarafa ya Ukwama na Lupalilo ulifanyika ambapo
Vijiji 20 viliwezeshwa kuandaa mipango
ya matumizi ya ardhi na hati miliki za kimila 287.
0 Maoni