KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE: Kauli ya kutangaza vita na Amini

 

Nyerere atangaza rasmi vita na Idi Amin ukumbi wa Karimjee

'Sisi kama wanachama halali wa umoja huu tulitaka jambo moja tu lifanyike na nilimjulisha Mwenyekiti wetu wa OAU Rais Jaffeir Nimeir wa Sudan kuwa Amin amefanya jambo la makusudi na mimi naliita la makusudi kabisa kwamba ameingia Tanzania ambayo ni taifa huru akachukua sehemu ya kipande cha ardhi ya Tanzania akaikalia kimabavu, tukaijulisha OAU kwamba tunachotaka sisi ni jambo dogo sana kwamba OAU itoe tamko la kumlaani tu Amini kuwa kitendo hiki si cha kiungwana hata...hata kidogo. Sasa madhali OAU iliamua kukaa kimya leo nimekuja kuwaambieni kuwa sasa tunaitangazia Dunia kuwa Tanzania tunayo kazi moja tu kuwa ni kumpiga Amin; uwezo tunao, sababu tunayo na nia tunayo. Tunaomba mataifa marafiki wasituambie kuhusu suluhu bali wajue kuwa tunayo kazi hii na ikibidi waje watusaidie'

Dk. Julius Kambarage Nyerere Oktoba 1978 Karimjee Hall.

Chapisha Maoni

0 Maoni