Israel yatanganza kuwa tayari kwa vita na Palestina

 

Israel imetangaza kuwa tayari kwa vita baada ya makumi ya Wapelestina wenye silaha wa kundi la Hamas kushambulia kusini mwa Israel kutokea ukanda wa Gaza.

Video iliyosambazwa kwenye mitandao ya jamii, inaonyesha wapiganaji wa Kipalestina wakiwafyatulia risasi wapitanjia mitaani katika mji wa Sderot huko Israel.

Pia kombora la roketi la Palestina lililorushwa kutokea ukanda wa Gaza, limesababisha kifo cha mwanamke mmoja raia wa Israel.

Taarifa zinasema makombora 7,000 yamerushwa na Hamas kutoka Gaza kushambulia Israel, katika tukio ambalo limeishangaza dunia.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, amesema kwamba “Hamas wamefanya kosa na wamenzisha vita dhidi ya nchi yake.”

Taarifa zaidi zinasema kwamba Israel imeshaanza mashambulizi ya anga ili kujibu mapigo katika maeneo mbalimbali ya Gaza.

CHANZO: BBC 

Chapisha Maoni

0 Maoni