Israel yasema bado ipo kwenye vita na kundi la Hamas

 

Jeshi la Israel limesema bado kunamapigano katika maeneo nane ndani ya nchi hiyo, siku moja baada ya wapiganaji wa Hamas kuingia Israel kutokea Gaza.

Msemaji wa Jeshi la Israel amesema kwamba bado wapo vitani, bado wanafanya jitihada za kuweza kutwaa umiliki wa maeneo ya Israel kutoka kwa Hamas.

Mamlaka za Palestina zimesema mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua Wapalestina 313 katika ukanda wa Gaza na kujeruhi watu waoatao 2000.

Nchini Israel nako watu 300 wameuawa na makumi ya raia wa Israel wametwaliwa mateka na wapiganaji wa kundi la Hamas.

Jana Jumamosi, Hamas walianzisha mashambulizi ya makombora ya roketi 7000 na wapiganaji wake kuingia Israel, katika shambulizi kubwa kuwahi kufanywa katika miongo kadhaa.

Chapisha Maoni

0 Maoni