Dk. Mwinyi aagiza kiwanda cha kusarifu dagaa kikamilike Desemba 08

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amekagua miradi miwili akianzia mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusarifu dagaa cha ZAFICO na amewaagiza Jeshi la Kujenga Uchumi-JKU ambao ni mkandarasi kuwalipa fidia wananchi waliovunjiwa vibanda vyao.

Dk. Mwinyi amewapa JKU hadi tarehe 08 Desemba mwaka huu wawe wamekamilisha ujenzi wa mradi huo atatembelea tena maendeleo ya ujenzi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi akizungumza na wananchi katika eneo la mradi Wilaya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi, ameagiza walipwe fidia zao na atafuatilia kuhakikisha wanalipwa stahiki zao haraka wakiwemo vibarua waliolalamika kucheleweshewa malipo yao.

Baadae Dk. Mwinyi akatembelea mradi wa bandari kavu Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi. Eneo hilo linatumika kuhifadhi na kutoa makasha au makontena.

Chapisha Maoni

0 Maoni