Dk. Biteko kumuwakilisha Rais Samia Sherehe za Uhuru wa Uganda

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto Mashaka Biteko leo Oktoba 8, 2023 ameondoka nchini kuelekea nchini Uganda.

Mhe. Dk. Biteko ameenda Uganda kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa nchi hiyo.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Kesho Oktoba 9, 2023 nchini humo.

Chapisha Maoni

0 Maoni