Dawa ya kuongeza matiti yasababisha vifo vya mabinti mapacha

 

Watoto wawili ambao ni mapacha wenye umri wa miaka 17 wakazi wa Kijiji cha Bubale katika Kata ya Nkololo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya kupewa dawa na mganga wa jadi kwa lengo la kuwaongezea ukubwa wa matiti ili waweze kuolewa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Byuna ameeleza kuwa mganga huyo anaitwa Masunga Tumolo na majirani wamekiri kuwa watoto hao walikuwa kwa mganga huyo Kijiji cha Byuna ambako walikwenda kuoga dawa ya kuwaotesha matiti.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Byuna, Dkt. Deogratius Mtaki amesema awali alipokea mwili wa Dotto na baadae akampokea Kulwa akiwa mahututi baada ya muda mfupi naye akapoteza maisha.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga ambaye alifika katika eneo la tukio hilo amekemea kitendo hicho na kulitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na tukio la mauaji ya mabinti hao.

Chapisha Maoni

0 Maoni