Zoezi la upigaji kura uchaguzi mdogo Mbarali lakamilika salama leo

 

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali, Bw. Missana Kwangura amesema shughuli ya kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo imemalizika salama na kwamba kinachoendelea kwa sasa ni kazi ya kuhesabu kura kwenye vituo vyote 490 vya kupigia kura na kuwasilisha matokeo ya vituo kwenye kituo cha kujumuisha na kutangaza matokeo.

Bw. Kwangura amevitaka vyama vya siasa, wagombea na wapiga kura kuwa wavumilivu wakati kazi ya kukusanya matokeo kutoka vituoni ikiendelea na kwamba matokeo yatatangazwa mara baada ya kukamilika kwa kazi ya majumuisho ya kura.



Chapisha Maoni

0 Maoni