Gwiji wa Bollywood Sanjay Dutt atua nchini kufanya Royal Tour

 

Msanii maarufu duniani kutoka kwenye kiwanda cha filamu nchini India maarufu kwa jina la Bollywood, Sanjay Dutt, akiwa na filamu zaidi ya 200 na tuzo zaidi ya 23 na akiwa mwaka jana 2022 ametajwa kuwa mmoja wa wanafilamu 3 wa India wenye mauzo mengi (Highest Grossing Indian Films), baada ya kuwasili nchini jana sasa leo anaanza rasmi “Royal Tour” kwa kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini Tanzania.

Wakati baadhi ya waigizaji aliowakuta wa zama hizo katika kiwanda cha Bollywood kama Mithun Chakroboti, Amita Bahchan, Shakti Kapoor na Govinda, wakiwa wameondoka katika kiwanda hicho, Sanjay bado amesimama juu kilele akiwa na akina Shah Rukh Khan kupeperusha kiwanda cha filamu za India na hivi karibuni jarida la Filmfare lilimtaja katika 20 Bora ya “100 Years of Hindi Films.”



Chapisha Maoni

0 Maoni