TANAPA yanadi vivutio vya utalii Maonesho ya Kimataifa Arusha

 

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linashiriki katika Mkutano na Maonesho ya Kimataifa Arusha yanayofanyika katika ukumbi wa Gran Melia katika kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani.

Vivutio na shughuli za Utalii pamoja na Fursa za Uwekezaji ni miongoni mwa mambo ambayo wageni waliotembelea katika meza ya TANAPA walipata fursa ya kuhabarishwa.

Aidha, Naibu Kamishina wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara Herman Batiho ambaye alihutubia mkutano wa maonesho hayo alipata fursa ya kutembelea meza ya TANAPA.



Chapisha Maoni

0 Maoni