Real Madrid yapata ushindi kwa tabu dhidi ya Union Berlin

 

Jude Bellingham ameifungia Real Madrid goli katika dakika za mwisho na kuipa ushindi dhidi ya timu ngeni katika michuano ya UEFA ya FC Union Berlin katika dimba la Santiago Bernabeu.

Kwa goli hilo Bellingham anafikisha magoli sita katika michezo sita aliyoichezea Real Madrid tangu ajiunge na klabu hiyo katika kipindi cha uhamisho cha majira ya joto. 

Timu ya Manchester United wameendelea kupokea vipigo baada ya kujikuta wakifungwa magoli 4-3 dhidi ya Bayern Munich, huku kipa wao Andre Onana akijibebesha lawama za kipigo hicho.

Chapisha Maoni

0 Maoni